JWTZ LAKANUSHA TUHUMA ZA UBAKAJI MTWARA


 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)limepokea taarifa kwamba waandishi wa Habari kadhaa wamepelekwa Mtwara kwenda kumhoji msichana mmoja kwa madai ya kubakwa na wananjeshi wa JWTZ.
JWTZ  linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa endapo taarifa hizo zitatangazwa kwenye baadhi ya vyombo vya Habari wazipuuze kwani hazina ukweli  wowote zaidi  ya kuwa ni za upotoshaji.
Msichana huyo amepandikizwa ili kuharibu taswira nzuri ya JWTZ. Ifahamike kwamba maafisa na askari wa JWTZ waliopo huko Mtwara wanafanya kazi kwa uangalizi wa karibu na vitendo hivyo vya aibu hawawezi  kuvifanya. 
Jeshi letu linafanya kazi kwa nidhamu na si kama baadhi ya watu wenye maslahi binafsi wanavyolipaka matope.
Tunapenda kuwafahamisha watanzania wote kuwa JWTZ lipo kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote.
Tunasikitika sana kama wapo watanzania wenye mawazo hayo machafu ya  kulichafua JWTZ lenye sifa nyingi ndani na nje ya nchi yetu.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 92023, Simu: 0764 742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

0 comments:

DENTI APEWA KICHAPO NA WAZAZI WAKE KWA KUKUTWA GESTI

Mwanafunzi mmoja amefumaniwa katika nyumba moja ya wageni (guest house) hapo jana, tarehe 29/6/2013 majira ya saa nane mchana katika eneo la Yombo Vituka jijini Dar es salaam.

Hata hivyo mfumaniwa mwenzake  ( mwanaume ) hajakamatwa kwani aliponyoka na kukimbia.

Wazazi wenye  uchungu na hasira wakiwa na binti yao mara baada ya fumanizi.
Wazazi wakimpiga binti yao kwa uchungu na hasira mara baada ya fumanizi.
(Picha zote na maelezo yameletwa na Dei Misana- Wavuti.com)

0 comments:

Govt ready to switch off unregistered cell phones


Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA)


Come July 10, 2013 all unregistered SIM Cards will be phased out the National Assembly has been told.

In her supplementary question Lolensia Bukwimba (Busanda-CCM) wanted to know what measures the government was taking against agents registering Sim Cards without identity cards of their customers and as a result customers used the loophole by registering fake names.

Responding to the question Deputy Minister of Communication, Science and Technology, (Bumbuli CCM) January Makamba, said the government had entrusted the responsibility of registering SIM Cards to telecommunication companies, however, some of them were unfaithful.

Makamba said further that because some agents were selling unregistered SIM Cards, some customers used the loophole by registering fake names and eventually using their unregistered Sim Cards to involve in crime.

However, the minister said when the National Identity Cards become in use, there will re-verify the cards used to register Sim Cards to contain people who cheat in the course of registration.

In another development, Makamba said it was acceptable to give ones mobile number to another person, but the problem will be for that person to misuse that number by uttering abusive language, theft or other forms of crime.

In her basic question Dr Getruda Rwakatare (Special Seats) wanted to know what measures the government was taking to put to task culprits who send abusive messages to people.

The government through the Communications Regulatory Authority (TCRA) had managed to register until now about 21,403,699 SIM Cards across the country, Makamba said.

However, he said despite the registration of Sim cards, some people continue misusing mobile phones, according to Makamba.

The government allows customers to use their mobiles 30 days without registration. Some agents reportedly sell SIM Cards without registering them, taking the loophole to use fake names.

In a week-long survey early this year The Guardian found that SIM card vendors and customers alike could sell and buy chips without necessarily registering them and play all sorts of unlawful acts, including using them for abusive purposes, theft and other forms of crime.

The Guardian also found that one can buy the chip and start using it before registration and in case they decide to register it, they still can use false names as presentation of identities is not obligatory.

The Guardian has also established that SIM card vendors can also furnish false information to the mobile phone operators -- false identity cards to have the customer registered.SOURCE: THE GUARDIAN

0 comments:

Obama ajibu mapigo kutoitembelea Kenya


obama30_300_172
WAKATI RAIS wa Marekani, Barack Obama amesema asingeweza kufanya ziara Kenya kutokana na Rais wake, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Rutto kukabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), pia amehadharisha Afrika kuhakikisha kuwa kampuni za kigeni zinaajiri wafanyakazi wazalendo ili wawekeze nchini mwao.
Alitoa kauli hizo mbili kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na baadaye alipozungumza na viongozi vijana wa Afrika akiwa katika ziara yake nchini Afrika Kusini.
Akizungumza jioni jana na vijana katika eneo la Soweto jijini Johannesburg, Obama alisema ataangalia uwezekano wa kwenda Kenya akiwa bado madarakani kwani bado ana miaka mitatu na miezi saba ya uongozi wake.
Alisema hayo alipojibu swali la mmoja wa vijana wa Kenya waliokuwa wakifuatilia kwa njia ya televisheni, aliyetaka kujua sababu ya yeye kutokwenda Kenya katika ziara hii.
Akifafanua, alikiri suala la Mahakama ya ICC nalo limechangia kutokana na kwamba ni suala la kimataifa. “Mnakumbuka nilifanya ziara ya Ghana mwaka 2009 na safari hii nilitaka nifike pia Kusini mwa Afrika na Tanzania nilishapanga muda mrefu … Kenya nilishafika mara nyingi kwa kuwa ni nyumbani, lakini nitakuja tena,” alisema Obama.
Alipongeza uchaguzi wa Kenya safari hii, ambao alisema uliendeshwa vizuri bila kusababisha ghasia kama uliotangulia. Kabla ya kujibu swali hilo alisalimia “hamjambo” na kumalizia na “ahsante” baada ya kuulizwa swali hilo.
Alisema ni vigumu kwake kutembelea nchi ambayo Rais wake (Uhuru Kenyatta) na Naibu wake (William Ruto) wanashitakiwa katika Mahakama ya ICC.
Kenyatta na Ruto wanakabiliwa na mashitaka katika Mahakama hiyo, kwa madai ya kushiriki ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, ambazo zilisababisha vifo vya watu 1,300 na wengine kadhaa kukosa makazi.
Mapema jana, akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari katika mkutano wake na Rais Jacob Zuma, kama Marekani inajisikia kutishika na ongezeko la mataifa mengine kuelekeza uwekezaji katika Afrika, kama vile China, alisema yeye kama Rais wa Marekani anaamini uwekezaji huo si tishio kwake kwani ni jambo zuri kwa maendeleo ya bara la Afrika.
Alimpongeza pia Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na kumwelezea kama “mfano wa kuvutia kwa dunia”. Alisema hayo baada wawili hao kufanya mazungumzo ya faragha kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Hata hivyo, mapema Obama alisema hataweza kukutana na Mandela (94) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Medi-Clinic ambako anasumbuliwa na matatizo ya kupumua na hivi sasa anapumua kwa msaada wa mashine.
Badala yake ilipangwa Obama aonane na familia ya kiongozi huyo, ambapo yeye na mkewe Michelle watatoa salamu zao ikiwa ni pamoja na fikra na maombi yao katika kipindi hiki kigumu kwa Mzee Madiba na familia yake.
Zuma alisema kiongozi huyo bado hali yake ni mbaya, lakini alikuwa na “kila matumaini kwamba atatoka hospitali muda si mrefu.”
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye ndege akitoka Senegal juzi, Obama alisema: “Kitu cha mwisho ninachotaka kufanya ni kutojiingiza kwa wakati huu katika masuala ya familia kuhusu hali ya Mandela.
“Nadhani ujumbe mkubwa tunaotaka kuutoa si moja kwa moja kwake, lakini kwa familia yake – ni pongezi kwa uongozi wake wa miaka yote hiyo, na kwamba fikra na maombi ya watu wa Marekani yako kwake, familia yake na nchi yake.”
Mkewe wa zamani, Winnie Madikizela-Mandela, alisema jana, kwamba isingekuwa haki kwa Obama kumtembelea Mandela akiwa katika hali mbaya vile.
“Mimi si daktari, lakini naweza kusema kwamba kutokana na jinsi alivyokuwa katika siku chache zilizopita, kuna maendeleo makubwa, lakini kitabibu bado hali yake si nzuri,” alisema Winnie.
Obama kwa mara ya kwanza alikutana na Mandela mwaka 2005 alipokuwa bado Seneta wa Marekani. Wawili hao wakaja kuwa marais wa kwanza weusi wa nchi zao na wote walipokea nishani za amani za Nobel.
Mkewe Michelle na mabinti zao Sasha na Malia, walipata kukutana faragha na Mandela mwaka 2011. Rais huyo wa Marekani alimwelezea Mandela kama shujaa wa dunia, ambaye matendo yake yatadumu kwa vizazi vingi na ndiye ‘alimshawishi’ kuingia katika uanaharakati akiwa mwanafunzi.
Ugonjwa wa Mandela hata hivyo umegubika ziara hiyo ya Obama ambayo ilipangwa muda mrefu kabla Mandela hajakimbizwa hospitalini na ililenga kushughulikia zaidi biashara na maslahi kwa mataifa hayo mawili makubwa.
Zuma alisema katika miaka ya themanini, Obama alihusika katika kampeni za kuiwekea vikwazo Afrika Kusini ya Ubaguzi, lakini hivi sasa ni muda wa kuondoa fikra hizo na “kuwekeza upya .”
Wakati Afrika Kusini ikikosolewa kwa kuwa na ukuaji uchumi wa polepole wakati nchi zingine za Afrika zikienda kwa kasi, Zuma alikanusha hilo akisema: “Tunatekeleza ndoto na sera za Nelson Mandela.” Alisema Rais huyo wa zamani hivi karibuni alimwambia: “Nikienda kulala, nitafurahi kwani najua nitaiacha Afrika Kusini ikisonga mbele.”
Obama jana alisema mfano wa Mandela wa “nguvu za kanuni, za watu kusimama kudai haki ni nini inaendelea kung’aa kama mnara wa taa”.
“Kumiminika kwa maombi ambako tumekuona katika siku za karibuni kunaonesha ushindi wa Mandela, na taifa lake linazungumza kitu kilichoko katika roho ya ubinadamu; kilio cha haki na hadhi ambayo inaondoa mipaka ya rangi na matabaka na imani kwa nchi,” alisema.
Zuma alisema kama viongozi wa kwanza weusi wa nchi zao, Obama na Mandela hawaepuki kuweka historia na hivyo “wanabeba ndoto za mamilioni ya watu wa Afrika na walioko nje ya Afrika ambao awali walikandamizwa.
Viongozi hao walizungumzia masuala mengi kwa upana katika majadiliano yao, ikiwa ni pamoja na biashara na viwanda, migogoro katika eneo hilo la Afrika, juhudi za kukabiliana na Ukimwi na masuala ya nje.
Zuma alisema ziara ya Obama imekuja kwa wakati mwafaka, ambao unashuhudia soko la Afrika Kusini likikua na alishawishi uwekezaji zaidi kuja nchini humo kutoka Marekani.
Pia alisema anaamini chama cha ANC, ambacho ndicho tawala kikiwa kimeanzishwa na Mandela, kinaendelea “kufuata nyayo” za kiongozi huyo wa zamani.
“Sina shaka kwamba ambacho tumekuwa tukikifanya ni sehemu ya ambacho Mandela angekuwa anafanya kama angekuwa hapa,” alisema.
Obama, ambaye anafuatana na familia yake aliwasili Afrika Kusini juzi jioni akitoka Senegal. Jana na leo alitarajiwa kutembelea kisiwa cha Robben kilichoko Cape Town ambako Mandela alifungwa miaka 18. Jumatatu ataendelea na ziara yake Tanzania.
Kuhusu kufuatana na familia yake, Obama ambaye na mkewe wana asili ya Afrika, alisema anafanya hivyo ili kuwafundisha historia ya Afrika na ndiyo maana akawapeleka kisiwa cha Goree, Senegal kuona historia ya utumwa na Robben kuona alikofungwa Mandela.
Mandela anakumbukwa kwa kuongoza mapambano dhidi ya utawala wa weupe wachache Afrika Kusini na kisha kuhubiri maridhiano licha ya kufungwa kwa miaka 27 jela. Alitunukiwa Nishani ya Amani ya Nobel mwaka 1993 na kuchaguliwa Rais mwaka uliofuata.
Aling’atuka mwaka 1999 baada ya kuongoza kwa kipindi kimoja. Alijiondoa katika maisha ya shughuli za kijamii mwaka 2004 na amekuwa akionekana kwa nadra katika matukio rasmi tangu wakati huo.
Ana historia ndefu ya matatizo ya mapafu, na aligundulika kuwa na kifua kikuu katika miaka ya themanini akiwa kifungoni kisiwani Robben.
Baada ya kuachiwa, Mandela alisema ugonjwa huo yawezekana ulisababishwa na unyevu ndani ya rumande alimokuwa akiishi. Obama pia anatarajiwa kukutana na Askofu Mkuu Desmond Tutu na kutoa hotuba katika Chuo Kikuu cha Cape Town leo usiku.

via Dar24.com

0 comments:

JK amgeuka Warioba


    
     RAIS Jakaya Kikwete amemgeuka Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kwa kuridhia azimio la Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutaka uwepo muundo wa serikali mbili. Rais Kikwete ambaye juzi aliongoza kikao cha Kamati Kuu (CC), mjini Dodoma, aliridhia azimio hilo, huku akijua fika kuwa ndiye aliyemruhusu Jaji Warioba kuingiza kipengele hicho kwenye rasimu wakati alipoifikisha mbele yake kabla ya kuitoa hadharani. Kutoka na hali hiyo, Kamati Kuu imewataka wanachama wao wote kupitia mabaraza ya CCM kuhakikisha wanakubaliana na msimamo wa chama wa kupinga muundo wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba.

      Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Zanzibar, waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa Kamati Kuu imepitisha azimio la kutaka mabaraza ya Katiba ya chama hicho yajadili na kuridhia msimamo wa kuwa na serikali mbili. Kamati Kuu ya CCM imekuja na mapendekezo ya namna ya kurekebisha kasoro kubwa za Muungano ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikiwa na Wazanzibari. Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa baadhi ya wajumbe wa CC kutoka Zanzibar walimshambulia Jaji Warioba kwa jinsi alivyoingiza suala la serikali tatu katika rasimu huku akiujua fika msimamo wa CCM.

      Hata katika mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulhaman Kinana na wabunge wa chama hicho uliofanyika mjini Dodoma, umesisitiza suala la serikali mbili tu. Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika mjini Dodoma, zilisema kuwa wabunge nao walichambua kasoro nyingi za rasimu hiyo, kubwa kuhusu muundo wa muungano na mipaka yake. “Kwenye mkutano wetu jana, tulikubaliana na msimamo wa Kamati Kuu wa serikali mbili na ndio ujumbe tunaupeleka kwa wananchi mikoani,” alisema mbunge mmoja alipozungumza na gazeti hili. Mbali ya rasimu ya Katiba, Kamati Kuu ya CCM ilimshangaa Jaji Warioba kwa kupitisha sifa za wagombea urais na wabunge ambazo zinaweza kuleta mkanganyiko mkubwa siku za baadaye.

      Katika mapendekezo ya rasimu kuhusu sifa za mtu kuwania ubunge, moja ya pendekezo hilo linasema kuwa, ikiwa “mtu huyo aliwahi kuwa mbunge kwa vipindi vitatu vya miaka mitano mfululizo, anapoteza sifa ya kuwa Mbunge.” Katika sifa za kuwa rais, inasema, “ili uwe rais, lazima uwe na sifa za kuwa mbunge. “Hivyo kama umemaliza muda wa kuwa mbunge, maana yake hutakuwa na sifa za kuwania urais kwa vile huna sifa ya kuwa mbunge. Huu ni mkanganyiko mkubwa sana,” alisema mmoja wa wajumbe wa CC.

Zanzibar yataka iwe na Benki Kuu yake


       Katika hatua nyingine, Baraza la Katiba Zanzibar (BAKAZA), limekuja na mapendekezo mapya kuhusu rasimu mpya ya Katiba ya Muungano. Katika mapendekezo hayo, BAKAZA limetaka Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano. Mapendekezo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa BAKAZA, Profesa Abdul Sheriff katika mkutano wake na vyombo vya habari. Mapendekezo mengine ni kutaka Benki Kuu (BoT), vyama vya siasa na uhamiaji yaondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano, pamoja na rasimu hiyo mpya kuzingatia utaratibu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano kupatikana kwa zamu kati ya washirika wa pande mbili za Muungano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

       Profesha Sheriff alisema mapendekezo hayo yametokana na uchambuzi wa rasimu ya Katiba ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa Juni 3, mwaka huu. Alisema hakuna sababu ya maana ya Polisi na Usalama wa Taifa kuendelea kubaki katika orodha ya mambo ya Muungano katika mfumo wa serikali tatu. Kwa mujibu wa mapendekezo hayo imeelezwa kuwa Ibara ya 217 ya rasimu ya Katiba ifutwe na kuruhusu kila mshirika wa Muungano kuwa na Benki Kuu yake itakayokuwa na mamlaka ya kusimamia sera za fedha pamoja na kuangalia mwenendo wa uchumi wa nchi husika, Tanganyika na Zanzibar.

      “Ni vema Zanzibar ikawa na mfumo wa sarafu yake na Benki Kuu yake ili iweze kudhibiti na kuendesha uchumi wake bila ya kuathirika na Muungano kama ilivyo kwa Hong Kong na Macau ndani ya Jamhuri ya Watu wa China,” alisema. Hata hivyo BAKAZA imesema kuwa kama suala la Mambo ya Nje litaendelea kubakia katika orodha ya mambo ya Muungano, basi nafasi za watendaji na mabalozi zitolewe kwa usawa Zanzibar. Mapendekezo hayo ambayo yanafungamana kwa kiwango kikubwa na msimamo wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Ibara ya 2 ya rasimu ya Katiba wametaka kuingizwa haki ya nchi mshirika wa Muungano kujitoa kwa kutumia utaratibu wa kura ya maoni, kama ataona hakuna manufaa yoyote katika muungano huo. Profesa Sheriff aliwaambia waandishi wa habari kuwa muhtasari wa mapendekezo hayo ndio utakuwa muongozo mkuu wakati wa kutoa elimu kwa wajumbe wa mabaraza ya Katiba katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Source: Tanzania Dama (June 2013). JK amgeuka Warioba. retrieved from Tanzania Daima

0 comments:

CHADEMA ngangari, Mbinu za CCM zagonga mwamba

 
KUIMARIKA kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kunazidi kuwachanganya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaotumia mbinu mbalimbali kukidhoofisha.
Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa licha ya viongozi wa CCM kuvitumia vyombo vya dola kuzima kasi ya CHADEMA, bado mambo yanaonekana kukiendea mrama chama tawala.
Hali ya mambo inaonesha kuwa CHADEMA inainyima usingizi CCM na serikali yake, ndiyo maana hivi sasa wameamua kukipaka matope kwa kutumia mbinu mbalimbali kuwafungulia kesi za ugaidi makada wao.
Uchambuzi wa kina wa matukio ya kisiasa ya hivi karibuni uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa kwa sasa CCM inakabiliwa na wakati mgumu kisiasa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya chama hicho.
Kuna viashiria vya wazi kuwa enzi za CCM kutawala siasa za Tanzania zinaelekea ukingoni kadiri CHADEMA inavyoimarika.
Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa CCM imeamua kulitumia Bunge na vyombo vya dola, ikiwamo polisi kufanikisha azima yao ya kuidhoofisha CHADEMA.
Jeshi la Polisi limekuwa likituhumiwa na viongozi wa CHADEMA na wananchi kuwa linatumiwa kuanzisha vurugu zinazosababisha mikutano ya CHADEMA kuvurugika au kutokea vurugu.
Vurugu hizo zinaelezwa ni mipango maalumu ya kukipaka matope chama hicho kikuu cha upinzani nchini mbele ya umma ili wasikichague kwenye chaguzi zitakazofanyika mwakani na mwaka 2015.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wameanza kupata hofu juu ya mwenendo wa Jeshi la Polisi katika mikutano ya CHADEMA ambayo mara nyingi risasi na mabomu ya machozi hutumika.
Agosti 27, mwaka jana polisi walizuia na kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wakielekea kwenye mkutano uliopigwa marufuku.
Katika purukushani hiyo kijana mmoja aliyekuwa akiuza magazeti mjini Morogoro aliuawa kwa risasi ingawa polisi walidai alipigwa na kitu kizito nyuma ya kichwa chake.
Septemba 2, jana mkoani Iringa, polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi kukabiliana na wafuasi wa CHADEMA na mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, alilipuliwa na bomu. 
Viongozi na wanachama wa CHADEMA walikusanyika katika ufunguzi wa tawi la chama chao katika Kijiji cha Nyororo, mkoani Iringa.
Kumekuwapo juhudi za makusudi za polisi na CCM kujaribu kuihusisha CHADEMA katika matukio yote mawili ya mauaji kwa lengo la kukichafua lakini bado upepo unaonekana kuvuma vibaya kwa watawala na vyombo vya dola.
Tanzania Daima, Jumapili, limedokezwa kuwa mkakati wa pili unaotumiwa na CCM dhidi ya CHADEMA ni kuwabambikiza kesi za ugaidi viongozi wake ili chama hicho kionekane hakifai mbele ya Watanzania. 
Machi, mwaka jana, Mkururgenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, alionekana kwenye mitandao ya kijamii akipanga kile kilichodaiwa na polisi na CCM kuwa mpango wa kumteka na kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications, Denis Msacky.
Baadaye Lwakatare akashtakiwa mahakamani kwa tuhuma za ugaidi na kesi hiyo ikaanza kutumiwa kisiasa na makada wa CCM ili kuidhoofisha CHADEMA.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, alikiri kufahamu watu walioiandaa video hiyo na kuiweka kwenye mitandao.
Kama ilivyokuwa kwa mipango mingine, mpango huu nao haukufua dafu baada ya Mahakama Kuu kumfutia Lwakatare mashtaka yote yaliyohusu ugaidi.
Kufutwa kwa mashtaka hayo kulikuwa pigo kubwa kwa CCM na polisi.
Harakati hizo zinaonekana kuzidi kushika kasi ambapo Juni 24 mwaka huu, makada wa CHADEMA wamefunguliwa mashtaka mengine ya ugaidi mkoani Tabora.
Makada hao wanatuhumiwa kumteka na kumdhuru kwa tindikali kada wa CCM wilayani Igunga mwaka 2011.
Washitakiwa hao ni pamoja na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, Evodius Justinian wa Bukoba, Oscar Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza na Rajab Daniel Kihawa wa Dodoma.
Watuhumiwa hao walisomewa shitaka la ugaidi kwa madai ya kumteka na kummwagia tindikali kada wa CCM, Musa Tesha, katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwaka 2011.
Juni 15, mwaka huu kulitokea mlipuko wa bomu katika mkutano wa CHADEMA wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani mkoani Arusha, ambapo watu wanne waliuawa na zaidi ya 70 kujeruhiwa.
Mara baada ya mlipuko huo viongozi wa CCM wamekuwa wakiihusisha CHADEMA na tukio hilo huku CHADEMA wakidai polisi na serikali ya CCM ndio wahusika wakuu.
Tukio hilo lilianza kuchukua mwelekeo wa kisiasa huku CCM wakionekana kutaka CHADEMA idhibitiwe katika mikutano yake ambayo imekuwa ikisababisha vifo na majeruhi.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema wanao ushahidi unaomuonesha aliyerusha bomu alikuwa ni askari na alilindwa na wenzake wakati akitoka uwanjani hapo.
Katika mwendelezo wa kuibana CHADEMA kwa kuwafungulia makada wake kesi zisizo na msingi, juzi polisi walimshtaki mahakamani Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, kwa tuhuma za kumtukana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Polisi walidai kuwa Mbilinyi maarufu kama Sugu alisambaza katika mtandao wa kijamii wa facebook ujumbe wa kumtusi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya kauli yake kwamba: “Wanaokaidi amri ya polisi wapigwe tu,” kuwa ni upumbavu.
Hata hivyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Dodoma ilitupilia mbali shtaka kutokana na hati ya mashtaka kukosa maelezo ya kutosheleza kuonesha kosa lililotendwa na Sugu, hivyo hati hiyo kukosa nguvu za kisheria.
Aidha, katika kuthibitisha kuwa viongozi wa CCM wamechanganywa na nguvu na ushawishi wa CHADEMA, uongozi wa Bunge nao umezidisha harakati zake za muda mrefu za kuwabana wabunge wa chama hicho kwa kuwazuia kuvaa suti za kombati ndani ya Bunge.
Kuzuiwa kwa mavazi hayo ambayo sasa yanatafsiriwa kuwa mavazi ya chama hicho, kunaelezwa ni ukiukwaji wa kanuni za Bunge.
Licha ya mbinu zote hizo, CHADEMA hivi sasa inaonekana kuimarika zaidi kwani katika uchaguzi wa udiwani uliofanyika hivi karibuni ilifanikiwa kuipoka CCM kata tatu.
Matokeo hayo yanatoa ishara kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa utaofanyika mwakani na ule mkuu utakaofanyika mwaka 2015, hali itakuwa ngumu zaidi kwa CCM.
Wadadisi wa masuala ya siasa wameweka wazi kuwa CCM imo katika hali ngumu kisiasa na haitashangaza kuiona ikishindwa vibaya katika uchaguzi mkuu ujao wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika mwaka 2015.
Kama CCM itashindwa katika uchaguzi mkuu ujao, basi itakuwa imefuata njia iliyopitwa na vyama vingine vikongwe katika Bara la Afrika, vilivyopigania uhuru wa nchi zao na ambavyo vimeondolewa madarakani na wanamageuzi kuanzia miaka ya 1990.
Vyama vikongwe Afrika vilivyowahi kuangushwa na wanamageuzi ni pamoja na chama kilichopigania uhuru wa Zambia cha UNIP chini ya Dk. Kenneth Kaunda, Chama cha Malawi Congress (MCP), kilichoongozwa na hayati Dk. Kamuzu Banda na Chama cha KANU kilicholeta uhuru wa Kenya, chini ya hayati Jomo Kenyata, ambacho kilitimuliwa madarakani mwaka 2002.

0 comments:

Ukweli kuhusu Rwanda, watutsi, Paul Kagame na uchochezi wa mch. MtikilaHabari wanaJF..!

Kwa muda sasa kumekuwa na mijadala mingi ikiilenga Rwanda, Paul Kagame na hususani kabila la Watutsi..!
Na hili suala limekolezwa zaidi na mch.Christopher Mtikilia ambaye ni mwanasiasa hodari hapa nchini Tanzania na pia ni
Mwenyekiti wa Chama cha DP.,kupitia waraka wake ambao mimi nauona ni wa kichochezi,uwongo,chuki na propaganda
Zisizokuwa za msingi ambao wenye malengo ya kupotosha ama kuleta uchochezi na mauji.

Najua kuna baadhi watapingana na mimi lakini kwa wale waliosoma historia watanielewa.

Nianze kwanza,..nini chanzo cha uhasama baina ya Wahutu na Watutsi..?
Kabla ya Ukoloni makabila haya mawili walishabihana na hata kuwa na lugha moja Kinyarwanda upande wa Rwanda
na Kirundi upande wa Burundi ingawa watutsi ndio walikuwa watawala kwakuwa walikuwa na utajiri mwingi wa ng'ombe maarufu "ankole" na hata pia tukiangalia hapa Tanzania Ufalme wa Karagwe ulikuwa na mchanganyiko wa Watutsi, Utawala wa Bachwezi na tawala mbali mbali kanda ya ziwa kulikuwa na mchangiko wa watutsi kabla ya ukoloni mwaka 1885..!
Wakoloni waliikiingi na Mkakati ulioitwa "Wagawanye na uwatawale".,na ulifanikiwa sana Kama nchini Nigeria baina ya Wakristo na Waislamu, Kenya baina ya wakikuyu na wajaluo,wakalenjin. ndio maana hata hapa Tanzania mikoa yenye wakristo wengi ilipata sana fursa ya elimu,miondombinu kuliko mikoa yenye waislamu wengi.

Tukija Rwanda huko zilianza taratibu za kuangalia pua,muonekano ambako waligawanywa kama Watutsi na Wahutu na hata kuvalishwa vibao.,ambako wale walioitwa watutsi walipewa fusra kubwa sana kwenye elimu na utawala na wakoloni ambao walikuwa wajerumani kisha wabeligiji..! mwanzo hawa watu walikuwa kama familia,ukoo na kabila moja paka kuweza kuwa na lugha moja na hata pia vinasaba vinaonyesha watutsi wana mchanganyiko na wenzao wahutu..!

Uhasama mkubwa uliibuka pale mwaka 1959,..ambako watutsi wengi walihamia Uganda,Congo na Hata Tanzania mpaka mwaka 1994 ambako yalitokea mauji ya kimbari na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000,000. kwa kifupi hii ndo historia fupi ya watutsi unaweza ukapata habari nyingi zaidi ya hapa.

Tuje kwenye waraka wa Mchungaji Christopher Mtikila,..ambao hauna tofauti na waraka uliosambazwa mwaka 1994 na
kusababisha mauji ya kikatili, wanawake na watoto kubakwa, miondombinu ya uchumi kuharibiwa vibaya..,na mtu kama huyu mahali pake hapa duniani ni Jela tena kifungo cha Maisha na hata peponi ni Jehanamu. ni kitu kibaya sana kuona Binadamu anapenda kuona vifo au mvurugano wa nchi ambayo sasa hv ina amani wakirudi tena katika mapigano. Mchungaji Mtikila ametumia mifano mfu na ya uongo kutetea hoja zake.

1.Suala la wafugaji kuingia bonde la Burigi, hili ni tatizo la serikali yenyewe kutolinda mipaka yake kuanzia maafisa uhamiaji, na hata kuliibuka baadhi ya tuhuma wafugaji kuonga wenyeviti wa vijiji ili waweze kupitisha ngombe. na hili suala limekuwa sugu sana, mfano tukiangalia hata kwenye ziwa letu Victoria Wakenya na Waganda wanakuja kuvua kwenye maeneo yetu na hata mbunge wa Ukerewe Mh.Machemli alishawahi kuja kulalamika bungeni, na hata baharini tukikumbuka wale samaki wa Magufuli walikuja kuvua kwenye mwambao wetu wa Bahari., hili tatizo la wageni kuvamia Rasilimali zetu ni Tatizo la Serikali kushindwa kulinda mipaka yake dhidi ya wavamizi ndio tatizo la wafugaji wengi kutoka Rwanda na Hata Burundi kuvamia maeneo yetu ya hifadhi. ndio maana imekalia kimya waraka wa Mch.Mtikila
kwani kwenye maeneo ya mipaka kuna tatizo kubwa sana la Rushwa.. na ningependa nimdahamishe Mch.Mtikila wanaovamia Rasilimali zetu sio tu watutsi hata pia Wakenya na Waganda ziwa Victoria,Wachina Bahari ya Hindi ni muhimu Serikali kuzidisa ulinzi kwakuwa wana Polisi na Jeshi.

2.Suala la Kagame Kupendeza Wanyarwanda 35,000. hivi nchi yetu haina usalama wa Taifa, haina idara ya uhamiaji, haina idara ya intelejensia polisi. kumbuka kuna makabila ya wahaya,waangaza,muha na wanzinza ambao wamenyangika na watutsi hata kabla ya Ukoloni mwaka 1885. na kumbuka nchi yetu imetoka uraia kwa baadhi ya wakimbizi kutoka makambini ambao walikuwa wahanga wa vita. ndio maana nchi kama Canada,Norway na Sweden wametoa uraia sana kwa wasomali ambako kwa akili ya mch.Mtikila angemaanisha wale wametumwa na Al shabaab. Mch.Mtikila hujui maana ya vita.

3.Suala la ''Black Apartheid" na kufanisha watutsi na nyoka., hapa sitaki kuongea sana lakini Mzungu ama Mhindi atamcheka sana Mwafrika kama anambagua mwenzake kisa kabila,ama rangi au dini.,

4.Mwisho ni nikija kwa PAUL KAGAME, Historia yake inasemakana amwaka 1979 alihshiriki vita ya TANZANIA dhidi ya nduli IDD AMINI DADA chini ya YOWERI MUSEVENI akiwa upande wa Tanzania kisha kushirikiana na Museveni mwaka 1985 ambako alikuwa mkuu wa Intelejensia wa jeshi la Museveni, hadi kujiunga na jeshi la Uganda Museveni alipokuwa Rais na kupelekwa Grand Rapids Nchini marekani kwa mafunzo zaidi ya Kijeshi, ambako aliiwezesha jeshi lake la RPF kutumia mbinu mbadala kuliteka jiji la Kigali dhidi ya serikali ya kipindi hicho.., Mchungaji Mtikila una habari kwamba WATUTSI wengi ambao wewe unawaita NYOKA walishiriki kwenye vita ya Ukombozi wa Watanzania mwaka 1979 dhidi ya IDD AMINI akiwemo hayati mtutsi FRED RWIGEYMA na hata baadhi ya Kufa kwaajili ya Taifa letu wakati wewe ukiwa kwenye handaki umejificha. mwenzio PAUL KAGAME alizaliwa ndugu zake wakichinjwa na kujikuta amekulia kambini., its fair kumuita muuaji bila ushahidi wakati wewe umefaidi matunda ya amani chini ya mtu unayemdharau Baba wa Taifa., think twice Mtikila huku ukikumbuka maumivu ya kupigwa jiwe huko Tarime kwa uchochezi wako.


Ningependa Watanzania Tusishabikie vitu visivyokuwa na Msingi wakati nchi yetu ikiwa na Matatizo makubwa ya Ajira,Afya,Umeme,Maji,Miondomb inu na N.k juzi wenzetu Brazil walipinga Matumizi makubwa ya maandalizi kombe la Dunia Nchini mwao,..sisi leo tunafurahia Serikali kupeleka Jeshi Nchini Congo.,wakati nyumba za Polisi zikiwa katika hali mbaya mfano zile kota za kariakoo msimbazi. ni masuala ya kujiuliza kitu gani kina faida nchini mwetu. kuna mtu hapa jamvini alitoa hoja watutsi watimuliwe nchini kwa msingi hiyo basi mikoa ya Kagera,Kigoma tuindoe kwenye ramani ya Tanzania kwani watutsi ni ndugu zao na hata lugha moja wanaongea. ikiwemo kirundi na kinyarwanda.

Tukiangalia Nchini zilizoendelea Kama MAREKANI,UMOJA WA FALME ZA KIARABU NA AFRIKA KUSINI, hizi nchi ni mchanganyiko wa mataifa mbali mbali, ww Mtanzania hujishughulishi anakuja Mkenya,Mnyarwanda anafanya maendeleo kwenye Nchi yako then unaaznisha maneno ya uchochezi wakati ni udhaifu wako wa kutojiendeleza. Tanzania ni nchi yenye rasimali kubwa sana ya ardhi lakini hatuitumii vizuri kuzalisha na kuongeza pato la Taifa kwanini wageni wasitutolee macho, mi naona waje tu kutusaidia kwasababu tumeshindwa.

via JF

0 comments:

MH. RAIS ZITAKAZOBAKI KWA OBAMA TUKUMBUKE NA SISI


BARUA YA MWALIMU Tanzania Nchi Yetu Sote KWA RAIS JAKAYA KIKWETE.

Habari yako mheshimiwa Rais?


Kwanza kabisa heshima yako, shikamoo na Pole sana na kazi za kulitumikia Taifa letu. 
Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi Matakapola, iliyopo Ilala hapa Dar. Haina haja ya utambulisho sana, naomba niende kwenye dhumuni la hii barua.(Ila ombi, naomba hii barua uisome wewe mwenyewe Rais, kama kuna servant hukusomea, aishie hapa. Aiweke store siku ukiwa na muda wa ziada wewe ndio uisome taratibu. 
Tafadhali sana. Ijumaa iliyopita mshahara wangu uliingia kwenye account yangu. Asante sana ingawa ni jasho langu. Basi yafuatayo ni matumizi yangu tokea Ijumaa hadi leo:

1. Kodi ya chumba (miezi 3)- Tsh 60,000, bili ya maji mwezi huu Tsh. 4,000 na ya umeme Tsh.5,000

2. Chakula cha akiba kwa huu mwezi (Unga 10kg, Mchele 10kg, Maharage 5kg, Mafuta 2Lts)-Tsh 42,000.
3. Mazaga zaga (Mazagazaga ni vitu vidogo vidogo ila vya muhimu sana) ya jikoni kama majani ya chai, chumvi, mkaa, kiberiti, mafuta ya taa-Tsh.10,000
4. Mwalimu usafi, imebidi nipitie mitumbani (huku ni sehemu unakoweza pata kitu cha bei kubwa kwa bei nafuu) nipate nguo za kubadilisha, maana hizi wanafunzi wamenizoea nazo. Hapa nili spend kama Tsh.15,000 na nikazipeleka kwa fundi kuzirekebisha Efect (Madhara) mojawapo ya nguo za mitumbani ni kawaida kuwa oversize, ombea isiwe undersize, na ukishanunua hakuna guarantee wala kurudisha) hapa nikatumia tena Tsh 5,000. Pia nikaenda duka la vipodozi kudaka body spray (Tsh.5,000), Mafuta ya BabyCare (Tsh.1000).
5. Wazazi wangu wameteseka sana kunisomesha, hivyo fadhila muhimu kuwarudishia kwa hiki hiki kidogo nipatacho. Nikawa M-Pesa Tsh.40,000 ili watumie kubadilisha mboga Juma pili na nusu iwasaidie kumalizia ada ya mdogo wangu Riziki, yupo ile shule uliyokuja izindua mwaka 2011/May/13 kijijini kwetu Mwankosi Mbozi Mbeya (au basi, sidhani kama unakumbuka, maana ulituahidi visima, barabara, madawati shuleni na kujenga bweni la wasichana, ila hadi leo umetuachia manyoya. Umekumbuka? Siku ile Ulivaa tai nyekundu, suti nyeusi na shati la drafti drafti jeupe. Na ulikuja na mama, yeye alivaa full vitenge vya chama! umeKumbuka?)
6. Kuna hela ya nauli kwenda na kurudi kila siku shuleni (Tsh.1000 per day), vitafunwa asubuhi kila siku (Tsh.200 per day), na vitu visivyo nunulika kwa wingi, maana vitaharibika kama vitunguu, sabuni, nyanya, nazi, karoti, nk nakadiria Tsh.10,000 kwa mwezi.
7. Mheshimiwa kuna vitu havizuiliki kama vocha, nyama wakija wageni, kwenda hospitali, bado kutoka out mara moja moja (Yaani kama wewe unavyoenda Sydney kula mbuzi, na sisi tunaenda kwa mama Lucy sinza, kula vifaranga au kuku mzima yani miguu,utumbo na kichwa)

8. Kuna hiyo pesa tunaiita hela ya emergency kama michango ya mtaani, sadaka, misiba, kiatu/nguo kwa fundi...etc. Mheshimiwa kama ulisoma vizuri hesabu kama mimi, roughly hapo ni jumla kama Tsh. 210,000 nikiongeza na pesa ya hitaji no.7&8 jumla kama Tsh.250,000. 


Mheshimiwa kutaja mshahara wangu hapa si vizuri, lakini, kwakuwa mama hapo nyumbani ameshawahi kuwa mwalimu naomba nikusumbue, hebu muulize walimu grade A, tunaoanza kazi tunalipwaje?

Kumbuka hapa bado niko peke yangu (Single Boy), sina hata mpenzi. Hivi nina ndoto za kuoa kweli ukitizama hicho kipato? Nikiwa na mtoto je? Akianza kusoma je? Nawaza sijui nikakope NMB au FINCA au VICOBA sijui Bay Port au SACCoS? Yaani sijielewi.

Sikushawishi uniongeze mshahara, ninachoomba tu, fananisha kazi yangu na hiyo wanayofanya wabunge "wako" niliowachagua, au hata kazi unayofanya wewe. Ndiyo. Wewe Mheshimiwa. 
Kuna watu wananishauri nianzishe tuition, lakini mimi ni mzalendo wa pili baada ya Nyerere, itakuwaje watoto wa maskini? Wasisome? Hapana, this is not fair (Sijui kama umeshawahi waza hili Mh.)
Wengine wamesema nianzishe biashara. Sijui hata pa kupata mtaji, pili sio vizuri maana nitaelekeza nguvu nyingi kwenye biashara kuliko kazi ya kuelimisha hili Taifa, narudia mimi ni Mzalendo. 

Hawa waliosema niache kazi  na kutafuta ingine kama naona hii ya ualimu hailipi wapotezee (achana nao). 

Ok Mh, naomba nisiongee sana maana una kazi, safari na mambo mengi sana hasa ukijumlisha na huu ugeni yani mpaka nakuonea huruma ila si ulituomba tukuchague ukatuahidi maisha..........basi naomba  nisikuchoshe.

Natumaini ombi langu  litasikilizwa na kufanyiwa kazi.

Wako katika kujenga, kuelimisha na kuandaa Taifa lijalo,

Mwl. Tanzania Nchi Yetu Sote

0 comments:

KWA UMAKINI HUU CHADEMA ITAFIKA MBALI SANACHADEMA wanafahamika kwa mipango madhubuti na makini. Viongozi wa JUU KABISA ndani ya chama wana sifa ya usiri na umoja. Mara nyingi pale wanapotoka hadharani kuiweka mipango yao huonekana kama maamuzi ya ghafla. Lakini huwa na mafanikio makubwa kama yalivyopangwa kutokea na hutokea kama walivyopanga yatokee. Kiufupi hakuna ughafla. Kwa wapinzani wao mafanikio haya huleta madhara makubwa sana na huwafika ghafla bila kutarajia. Hata ndumila kuwili ndani ya CHADEMA hupigwa na bumbuwazi jinsi mipango hii inavyofikia hatua za kutekelezwa bila wao kushiriki au kufahamu uwepo wa michakato yake. Moja ya bao la karne na mfano mzuri wa mikakati hii ni uteuzi wa Dr. Slaa kuwania Uraisi wa mwaka 2010. Jina lilifahamika siku iliyopangwa lifahamike hadharani na kuwaacha waasi wa ndani na wapinzani wa chama midomo wazi! Yaliyofuata ni historia ambayo wewe msomaji pia unaijua.

Kwa anayefanya tafakari vizuri atagundua kuwa wapinzani wa CHADEMA wanafamu fika kwamba hiki chama hakiwezi kumlengesha mapema mgombea wao ajaye au kuruhusu kwa namna yeyote ile akae pahala atakapolengwa na mashambulizi ya mara kwa mara kirahisi. Na yeyote anayeonekana kwa sasa wamemtengeneza tu ili wapinzani wa CHADEMA wapoteze risasi kwa kulenga wrong target. Watajichosha na kupoteza rasilimali zao wakidhani wanamdhoofisha mgombea ajaye kumbe wasijue wanajichosha wao wenyewe! Hii ni sababu ya kwanza.

Sababu ya pili, ni kanuni ya kawaida kwamba ukitaka kulitawanya kwa urahisi kundi ambalo uimara wake na umoja wake unachangiwa kwa kiasi kikubwa na umahiri wa uongozi wa mchungaji wake, basi piga mchungaji wao na wengine wote watatawanyika! CHADEMA inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa ndani ya chama. Hakuna dalili zilizowazi zinazoonesha taswira ya safu ya Uongozi ujao. Katika chaguzi zote zilizowahi kufanyika ndani ya CHADEMA kwenye ngazi yoyote ya juu zinadhihirisha kuwa ni vigumu kupenyeza mamluki au kuwavuruga kwa kutumia mamluki. Hii ni historia njema na inaweza kutumika kutuaminisha kuwa hata zamu hii watavuka salama. Kwa hiyo nafasi pekee kwa wapinzani wa CHADEMA kuleta mtikisiko ni kumuondoa Mchungaji wa kundi kabla ya muda wa ratiba ya kuondoka kwake.

Siamini kama kweli Freeman Mbowe amekuwa Mlengwa No. 1 wa dola ya CCM kwa pigo moja la ghafla na la bahati mbaya. Jipe muda kidogo kutafakari utaona jinsi pigo lilivyokuwa limepangwa kitambo na lilivyotakiwa kuwa moja tu lenye kufikia malengo makubwa kwa mkupuo bila kutikisa sana wala kuhamasisha hasira ya umma. Dondoo hizi zikusaidie:

Bomu maalumu na la teknolojia mpya kabisa kutoka kiwandani-China likaingia nchini na kulipuliwa ulinganishe na nguvu/jitihada inayowekwa na yombo vya usalama kujua liliingiaje nchini

Walenga shabaha (snipers) waliotayari kumalizia kazi iwapo bomu halikuleta madhara yaliyopangwa

Wapiga risasi wenye bunduki za kivita na zenye risasi za kutosha kuhakikisha blusters wanaondoka salama kwenye eneo la tukio
Mawasiliano kutokuwepo katika eneo la tukio nusu saa kabla na nusu saa baada ya tukio

Bado tunasubiri ushahidi wa video toka kwenye DVR hapo ndipo wabaya wote watafyata midomo kama ilivyokuwa kwa Daudi Mwangosi ambaye tulishaanza kuaminishwa kuwa alipigwa na kitu kizito toka kwa waandamanaji akikimbilia kwa polisi kumbe kitu kizito kilitoka kwa polisi wenyewe.

Halafu wengine wanasema eti walijilipua wenyewe kutafuta huruma ya wananchi kweli!? Tusemeje sasa na hayo ndio matokeo ya akili ndogo kuongoza akili kubwa.!

By: Tanzania Nchi Yetu Sote

0 comments:

ZIARA YA OBAMA- MAENEO YATAKAYOATHIRIKA


 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, SAID MECK SADICK, amesema serikali imechukua tahadhari zote katika kuhakikisha shughuli zote za wananchi za kibiashara zinaendelea kama kawaida wakati wa ziara ya rais wa Marekani Barack Obama.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema katika kipindi hicho wafanyabiashara kutoka mikoani na ndani ya jiji wataendelea kuingiza bidhaa zao katika masoko kama kawaida bila kuzuiliwa, na kwamba si barabara zote zitakazofungwa na kutolea mfano wa barabara itakayofungwa kuwa ni barabara ya Nyerere ambayo wageni wengi hutumia na kwamba ziara hiyo haitaathiri maonesho ya 37 biashara maarufu kama sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. JULIUS NYERERE.

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajia kuzuru Tanzania siku ya jumatatu ambapo miongoni mwa masuala atakayoangazia ni pamoja na kuhamasisha demokrasia na kukuza fursa za kiuchumi.

Maandalizi ya mapokezi ya Rais Obama yamezidi kupamba moto hasa katika jiji la Dar-es salaam ambapo ndipo kituo chake cha kwanza kwa rais huyo nchini Tanzania huku suala la usafi na matengenezo katika barabara nyingi Jijini likionekana kupewa kipaumbele tofauti na siku zote.
 
 

0 comments:

HIVI NDIVYO RAIS KIKWETE ALIVYOWAANDALIA MARAIS SHEREHE FUPI,MZIKI ALIUSAKATA PIA

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni zilizofadhli hafla hiyo.
 Mahali palipoandaliwa kwa dina kwenye viwanja vya Gymkhana
 Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika hafla ya chakula cha usiku.
 JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), King Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alnold Kilewo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Chibuku cha Dar Brew, Kilowi Suma (wa pili kushoto), katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete  kwa marais na viongozi mbalimbali waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kutoka kulia ni Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Halfan Mpango na Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Esther Mkwizu. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
 Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akihutubia katika hafla hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa marais na viongozi waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ilikuwa kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
 Bendi ya THT ikitumbuiza katika hafla hiyo
 Msanii Mwasiti akipongezwa na Mbunge wa Afrika Mashariki, Adam Kimbisa. Kulia ni Mbunge wa bunge hilo, Shy Rose Bhanji na Abdul Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge hilo.
                                              Kimbisa akiwa na Mwinyi, Bhanji na Richard Kasesera 
 
 
 
 
 
via HABARI MPASUKO 

0 comments:

Obama: Nipo tayari kumwona Mandela  • Taarifa za awali kuhusu ziara hiyo zilieleza kwamba Rais Obama hatamtembelea kwa kuwa haikuwepo kwenye ratiba.

Rais Barack Obama wa Marekani ambaye ameshaingia nchini Afrika Kusini amesema kwamba yupo tayari kumuona Nelson Mandela ikiwa familia yake itamkubalia.
Taarifa za awali kutoka nchini humo zilisema kwamba Barack Obama hataweza kumuona kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini ambaye amelazwa hospitalini.
Taarifa za Ikulu ya Marekani zilisema kwamba kiongozi huyo suala la kumuona Mandela lipo mikononi mwa wanafamilia ya mzee huyo.
Rais wa Marekani Barack Obama alipokuwa Senegal alisema kwamba ikiwa mzee Nelson Mandela atafariki dunia ushujaa wake bado utaendelea kubakia na kukumbukwa.
Alisema kwamba ushujaa wa Madiba utabakia milele, na kwa sasa anatakiwa kuombewa , hivyo sala zinahitajika kwa kila mtu ulimwenguni.
Obama alidhibitisha wiki iliyopita kwamba bado mpango wake wakuzuru Afrika Kusini upo pale pale licha ya kusikia taarifa a kuugua kwa Mandela.
Leo Obama atatembelea gereza la Robben gereza ambalo alifungwa kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini, pia atatembelea Soweto na atatembelea sehemu mbalimbali za Cape town.
Obama atahitimisha ziara yake hiyo kwa kuzungumza na baadhi wa viongozi wa nchi na wananchi wa Afrika Kusini katika Chuo Kikuu cha Cape Town.
Historia ya matatizo ya mapafu ya Mandela ilianzia tangu alipokuwa kwenye gereza la Kisiwa cha Robben karibu na Cape Town.
Aliachiwa huru mwaka 1990 baada ya miaka 27 na akaendelea kutumikia nchi kama Rais kuanzia mwaka 1994 hadi 1999.

via MWANANCHI 

0 comments:

Dk Mwakyembe, Nundu wachuana bungeni


  • Ni kutokana na Nundu kutaka kujua sababu za ATCL kupokonywa karakana yake ya matengenezo ya ndege iliyojengwa Uwanja wa Ndege wa Kiiimanjaro

Dodoma. Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, amekutana na wakati mgumu bungeni baada ya kubanwa na Waziri wa zamani wa wizara hiyo, Omary Nundu, aliyetaka kujua sababu za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupokonywa karakana yake ya matengenezo ya ndege iliyojengwa Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (Kia).
Nundu aling’olewa katika wadhifa huo Mei mwaka jana, baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri kufuatia shutuma za matumizi mabaya ya fedha zilizotolewa bungeni kwa wabunge takriban watano akiwamo Nundu.
Baada ya mabadiliko hayo, nafasi yake ilichukuliwa na Dk Mwakyembe ambaye awali alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.
Mvutano huo uliingiliwa kati na Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwa kumtaka Dk Mwakyembe kujibu kwa kifupi maswali aliyoulizwa na Nundu ambaye ni Mbunge wa Tanga Mjini, kwa maelezo kuwa wanajuana kwa viremba.
Katika swali lake la msingi, Nundu licha ya kutaka kujua sababu za ATC kupokonywa karakana na Kampuni ya Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (Kadco), alitaka maelezo ya idadi ya ndege zilikusudiwa kutengenezwa katika karakana hiyo tangu kukamilika kwa ujenzi wake mwaka 1979.
“ATC haikupokonywa karakana hiyo, ukweli ni kwamba uendeshaji ulihamishwa kutoka ATC kwenda Kadco mwaka 2000 kama sehemu ya maandalizi ya kubinafsisha ATC,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:
“Karakana ya Kilimanjaro ina uwezo wa kuhudumia ndege tatu kubwa aina ya Boingi 737 kwa wakati mmoja, wakati inajengwa ATC ilikuwa na karakana yake nyingine Kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere Dar es Salaam hivyo kushindwa kuitumia karakana ya Kia kikamilifu.”
Alisema karakana hiyo kwa sasa inatumika kutoa huduma kwa ndege za watu mashuhuri .
Katika swali lake la nyongeza Nundu alisema: “Majibu ya waziri (Mwakyembe) hayaridhishi, kwani ndege zilizokuwa zikihudumiwa katika karakana hiyo ni zile za 747 siyo 737.
“Pia Kadco imerudi serikalini miaka miwili iliyopita siyo mwaka 2000, nataka kujua karakana hii inatumikaje hivi sasa na Serikali ina mpango gani wa kuboresha matumizi yake?”
Baada ya mvutano huo, Spika Makinda aliingilia kati: “Nyie mlikuwa hukohuko na mnajuana kwa viremba, ila Mwakyembe nakuomba ujibu na muachane na hayo maneno yenu.”
Waziri Mwakyembe alisema: “Waziri aliyepita (Nundu) aliishia hapo na sisi wenzake tunaendelea kulimaliza hilo suala, natarajia baada ya kipindi kifupi tutakuwa tumemaliza jambo hili.”

via MWANANCHI 

0 comments:

RISALA YANGU INGEKUWA HIVI....

Kama ningeliteuliwa kuandika risala ya kumuaga RPC wa Iringa, basi ingekuwa hivi:

HONGERA SANA NDUGU KWA KUPANDISHWA CHEO NA HATA ALIYEKUPANDISHA CHEO PONGEZI NYINGI ZIMFIKIE.

MKE wa Marehemu Mwangosi, watoto, wazazi ndugu na jamaa bado wanakukumbuka na kidonda cha kuondokewa na mpendwa wao bado hakijapona. Hawana la kukufanya maana wao ni kama panzi mbele yako. Nyinyi ndiyo wenye nchi, mnayo mamlaka ya kudhuru mwili hata kuua bila kushitakiwa popote.
NAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA UTEKELEZAJI MWEMA WA MAJUKUMU YAKO MAPYA

0 comments:

MKETO WA CUF AHOFIWA KUFARIKI DUNIA AKIWA MIKONONI MWA JESHI-

Habari tulizopokea hivi punde ambazo bado hazithibitishwa zinadai kuwa Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF – Shaweji Mketo amefariki dunia baada ya gari walilokuwemo kukamatwa na wanajeshi wa JWTZ, inadaiwa kuwa wakati wakipelekwa Naliendele gari lilipata ajali na ndipo mauti yakawakuta, Idadi ya waliopoteza maisha bado haijajulikana.

Mwenyekiti wa CUF Lipumba inadaiwa kunukuliwa kuwa alipokuwa anajaribu kufwatilia suala hilo alijaribu kupiga simu ya Mketo kwa mshangao alipokelewa na mtu asiemjua huku akitoa matusi mazito.

 

via MEDIA 2 SOLUTION 


0 comments:

On The Eve of Presidential Visit: An Encounter with America – Open Letter to President Obama


Mr. President,
On the eve of you first visit to Tanzania I find myself called as if by fate or Providence to write this open letter to you as the leader of the Free World. In 2008 when your predecessor President George W. Bush made the first official visit by a sitting US President to the country I had the opportunity to write another open letter to him; it is in the same spirit I find myself writing this one. Welcome to the Beautiful Land of Tanzania where the natural beauty of the land is supernaturally paired to the charm of its people! Karibu Mr. President!
It’s an encounter of two unequal partners When an American President meets a Tanzanian President there would be an illusion that the two countries are somewhat equal – in any measure. It would be an illusion highlighted by the pomposity of the occasion but in all reality it’s would be an encounter or a meeting of sort of two – friendly – but unequal partners. On one hand the world only true superpower in all its economic, military and cultural spheres; on the other hand, one of the poorest nation on earth; economically a non-entity, militarily an irrelevant one; culturally a confused one.
Mr. President, think about this if you will- just for your amusement; US Federal budget is almost 4 Trillion US Dollars this year while that of Tanzania -passed few days ago – is only about 16 Billion US Dollars. To make a contextual comparison – the US defense budget is in the high ends of 500 Billion Dollars which makes the Tanzania national budget 31 times less than that of one US federal department. Even when comparing Tanzania’s national budget to that of the US Department of Agriculture budget still the Tanzanian national budget is dwarfed at the ratio of 1:9. So, Mr. President, when I say it’s an encounter of unequal partners I’m not just using some semantics; I’m stating a factual reality.
Forgive me Mr. President, I would describe the engagement or encounter between Tanzania and the US to be similar to an encounter between an elephant and an ant where by an ant has been led to believe- by the elephant mind you – that he was meeting an equal partner. This was said to be true simply because they both share the same jungle or share some common interests, interests that highly favor the elephant. In that encounter I pity the ant!
What happens after you leave?
Mr. President when you leave next week and you are back in DC much will be said in Tanzania of your visit. Some would say it was “highly successful” and “very beneficial” to the country and its people. I’m quite sure some of our elite and carrier politicians will speak of so many agreements that the US entered with Tanzania, or some aid package that you brought or a new program for Africa that the US pushed and Africans happily accepted. Indeed, to our ruling corrupt elite the success of your visit will only be described in terms of dollars! What you brought and how much your administration promised to Tanzania will be the only measure of the success of your visit and may be rightly so. But, is that the measure Tanzanians will use to gauge how beneficial your visit was to their lives and their daily experience in Tanzania? I’ll argue probably not.
A year after your visit or so, the Tanzanian people will look back and ask themselves whether their lives have been transformed for the better or they are still the same. I’ll propose to you Mr. President that your splendid visit will be considered to be a total failure if after few years from now the following areas in the life of Tanzanians would not show a tangible improvement:
1. Any improvement in the quality and infrastructure of education. With a literacy level at 70%, and a failed education system what would education system in Tanzania look after Obama’s visit? Well, I’ll bet none of the agreements (bilateral or private) entered between Tanzania and the US during your visit was targeted towards education reform.
2. Would there be any improvement in the protection of civil and human rights? I know you have made the issue of gay rights a cornerstone of your international aid policy. While this might make sense to you and your US supporters to a Tanzanian this has nothing to do with his or her daily experience. When it comes to human rights and civil rights Tanzanians would want to see how their security organs are reformed and how the government deal with political dissent. There is a bill now in the pipeline that would ban political demonstration in the country. If this bill passes then Tanzania would have gone to the politics of colonial era. Would the US support such a move? Would the US remain silent? Or, the US would only be vocal when it comes to the so called “gay agenda”?
Just to be on the record, Tanzanians have been very tolerant to their gay brothers and sisters. There is no lynching or even such homophobic attacks around the country that one would see in the US or Europe. The question of decriminalizing homosexual acts still remains the choice of the people. So far, I don’t think there is any case anywhere in Tanzania where a consensual gay people are facing criminal charges. However, there are a myriad of cases now pending or going on where political dissidents -some senior leaders in the opposition -are facing charges simply for exercising their civil rights.
3. How the Tanzanian government has reversed its troubling attitude and trend toward independent media. Last week the Committee for the Protection of Journalists – an International organization based in New York – wrote a letter describing the deteriorating freedom of the press in Tanzania. I’m quite sure the US Embassy has documented similar trend over the past few years. What would the situation be after a year since your visit? Will the Tanzania government supported by the US government continue with its assault of the free press?
4. In the past few years especially after the 2010 General Election the Tanzanian security organs (Police, Intelligence Service as well as Secret Branch) have continued to harass political opponents and some section of the press. We have seen what I would call as a politically compromised state organs acting with almost absolute impunity against the people. Last week’s order by the Prime Minister to the security organs to “beat up” any one considered to be a trouble maker or a threat to national peace instead of using legal tools came as a shock to some people. But to some of us who have noticed this trend it just confirmed our fears; the state organs in Tanzania are above the law and will act with absolute impunity against the citizens in the name of “safeguarding peace and tranquility”. If the kidnapping, torture and harassment of political opponents of the government continue unabated would we say a year from now that Obama’s visit was a huge success or we would lament the opportunity lost?
5. If a year or two years from now the majority of Tanzanians still live in primitive housing, in unplanned neighborhoods and continue to struggle with issues of energy, clean water and access to better health services then how can we praise your visit? Of course, by that time some American companies would have been awarded concessions in Rare Earth Minerals, Gas exploration, Uranium exploration etc. but what if all that means absolutely nothing to people who live in squatters? Well, The US and Tanzanian governments can sing about how much FDI has been injected in the country but what if it doesn’t change the lives of those people at the very bottom of economic and social status?
6. How corruption has been tackled in the country. Of all man-made calamities that faces Tanzania and unquestionably most part of Africa corruption stand alone in its impact, depth and stubbornness of defeat. Tanzania like many African countries is permeated in all levels of its government by corruption to the point that President Kikwete himself one time said that up to 20 percent of budget allocation ends up in corrupt hands; that’s about 3.2 Billion US dollars every year goes to corrupt public officials –some probably are at the forefront of you visit!. After your visit and before you leave office in 2016 what would be the level of public corruption in Tanzania?
Mr. President to me and possibly to many other Tanzanians it is in these areas that the success of your visit -the encounter with America – would be weighed against. When all is said and done, the Tanzanian people would look as if in rearview mirror your visit in the light of the positive impact it had made or not made in their lives. Not only would they say that when Obama came to Tanzania it was incredibly memorable even the famous Ocean Road was renamed to bear his name but also that the trajectory of national discourse was clearly positively and permanently altered.
Anything less than that would lead people to speak of your visit in terms of other hyped up visits and conferences of the past – such as the Sullivan Summit, the World Economic Forum, President Bush’s Visit, or President Xi Jinping’s Visit. This will be plainly true regardless whether there are countless contracts and agreements entered which would benefit the American worker. Your visit will be judged not by how many new jobs you created in America (of course my American friends will beg to differ) but by how many people were lifted out of the misery of condemning and perpetual poverty in Africa during your administration. President Bush actions helped reverse the HIV/AIDS trend in Africa and Africans will forever remember him for that; but yours will be judged even more pointedly.
As we marvel at the splendor and grandeur of America’s mighty displayed so marvelously at our present, as we admire a descendant of an African leading the world mighty power right in front of our eyes we hope and pray that the visit would impactful not just to this generation of Tanzanians but also to those yet born and their posterity. In Roman times when Caesar visited a land nothing remained the same for better or for worse, I hope your visit will not be remembered for the worst it had left behind. But if at the end only the Americans benefit and if only American companies reap the fruits of your visit then as I said above;
I still pity the ant. Karibu Sana MMM (BGM)
Detroit Michigan
USA


via Mwanakijiji

0 comments:

Utafiti: Umbea una faida kiafya 

  • Umbea ni kawaida na hauzuiliki, tatizo ni yaliyomo ndani ya umbea ambayo mara nyingi hutegemea na mawazo mtu aliyonayo. Kama ana mawazo hasi, ataongea mambo mabaya


Kama hujui, wanaume ni wambea zaidi ya wanawake, tofauti ni kwamba wao hawasutani hadharani!
Katika jamii yoyote mtu mwenye tabia ya umbea huchukiwa, hutengwa na hata wakati mwingine hupigwa kwa kuonekana kuwa ni chanzo cha migogoro na huku viongozi wa dini wakimwona mtu wa aina hiyo kuwa ni mtenda dhambi.
Watu wanaopenda tabia ya umbea huenda wakawa wamepata mtetezi. Ripoti iliyotolewa hivi karibuni kuhusu tabia ya watu kupenda kutumia muda mwingi kusema mambo ya watu wengine, inasema tabia ya umbea ina manufaa kiafya.
Ripoti hiyo iliyotolewa na watafiti kutoka chuo kikuu cha Rhode Island cha Marekani, inasema kuwa watu wanaonufaika zaidi za tabia hiyo ni wale wanaopenda kuongea mambo mabaya wa watu wengine kuliko wenzao wanaopenda kuzungumza kuhusu mambo mazuri.
Wataalamu hao wamebaini kuwa iwapo mtu atatumia dakika 20 kuzungumzia mambo mabaya ya watu wengine, anaweza kuimarisha afya yake kwa kupunguza msongo wa mawazo, woga na mashaka kwa asilimia 96 kwa muda wa masaa manne mfululizo.
Hata hivyo, wamebainisha kuwa mtu akitumia muda huo huo kuzungumza mambo mazuri ya watu wengine, atapunguza msongo wa mawazo kwa asilimia 72 ikimaanisha kuwa watu wenye kuzungumza mambo mabaya ndio wenye kunufaika zaidi.
Watafiti hao, wakifafanua hali hiyo wameelezwa kuwa mtu anapoongea habari nzuri zinazowahusu watu wengine huuchochea ubongo kutaka kujiunganisha na mtu anayezungumzwa, wakati yule anayezungumza habari mbaya huwa kinyume chake.
Mtu anayezungumza habari mbaya anatabia ya kutokuhifadhi alichokisema, bali huendelea na mambo yake kama kawaida, wakati anayezungumza habari nzuri hukaa nazo moyoni kwa kipindi cha muda fulani.
Mtaalamu wa Saikolojia kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Lusajo Kajula anasema binadamu wote huongea kuhusu watu wengine, lakini umbea ni zaidi ya maongezi.
Lusajo anasema asili ya mwanadamu ni kuzungumza japokuwa wakati mwingine hujikuta akiishia kutoa mifano halisi ya maisha ya watu wengine na hivyo kuingia katika mgogoro wakati mtu aliyesemwa anaposikia.
“Umbea ni kawaida na hauzuiliki, tatizo ni yaliyomo ndani ya umbea ambayo mara nyingi hutegemea na mawazo mtu aliyonayo. Kama ana mawazo hasi, ataongea mambo mabaya,” anasema Kajula.
Hata hivyo, Kajula anapingana na dhana iliyopo miongoni mwa watu kuwa mwanamke ndiyo anayependa zaidi tabia ya kuzungumza mambo ya watu wengine kuliko mwanaume.

via MWANANCHI 

0 comments: