. 

POLENI WALIMU

No Comments
NYONGEZA YA MSHAHARA MWAKA HUU JULAI 2013
Kutokana na barua yenye Kumb Na CAC.205/228/01/C/14 ya tarehe 2 Julai,2013, Kutoka Menejiment ya utumishi wa umma, inayohusu kupandisha mshahara kwa watumishi wa serikali yenye kichwa cha habari “WARAKA WA WATUMISHI WA SERIKALI NA. 1 WA MWAKA 2013, MAREEKEBISHO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA SERIKALI” Inasema Serikali inaendelea kutekeleza sera ya malipo ya mishahara na motisha katika utumishi wa umma mwaka 2010. Katika hatua za kutimiza malengo ya sera hii, serikali inafanya marekebisho ya mishahara ya watumishi wake kuanzia tarehe 1 julai, 2013. Kutokana na marekebishi hayo kima cha chini kitakuwa kutoka 170,000/= hadi tsh 240,000/= kwa mwezi. Mishahara ya watumishi wengine imeongezwa kwa wastani wa 8.41% . imesainiwa na KATIBU MKUU (UTUMISHI G.D.Yambeshi)(Mwisho wa kunukuu).
Barua hiyo ambayo inaonekana kuwa mwiba kwa watumishi wa kada ya UALIMU ambao walidhani serikali itajibu madai yao ya nyongeza ya mishahara, subira hiyo haijazaa matumaini kwani kwa mujibu wa waraka huo kada ya ualimu inaonekana iko nyuma ya kada za afya na kilimo. Hii ni sehemu ya waraka huo ukianisha madaraja ya mishahara mipya kuanzia julai 1, 2013.(N:B Kwa wale wasiojua ngazi ya mshahara ya B ni ya mwenye cheti (certificate), C= Diploma, D= Degree)
WALIMU
TGTS B1= 344,000/=
TGTS C1= 432,500/=
TGTS D1= 589,000/=
TGTS E= 769,000/=
TGTS F= 1,003,000/=
TGTS G= 1,320,000/=
Wakati kwa kada ya KILIMO mambo ni mazuri kabisa kama ifuatavyo
B= 1,060,000/=
C=1,252,000/=
D= 1,473,000/=
E=1,736,000/=
POLENI SANA WALIMU KWA KUENDELEA KUNYONYWA HAKI ZENU.
Katika waraka huu sehemu ya mwisho unasema
WARAKA HUU NI KUMBUKUMBU NA TAARIFA YA SERIKALI NA HAIRUHUSIWI KUTANGAZWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI