Tuesday, October 21, 2014


925356_1501548786777888_891361649_n
Ni leo asubuhi ndipo taarifa za msiba wa aliyekua msanii wa TMK Wanaume Family aliyekua akijulikana kama YP. Kwa mujibu wa maelezo aliyetoa Said Fella ambaye ndio kiongozi wa wanaume Family ni kua marehemu alianza kuumwa tangu mwezi wa nane mwaka jana. Na afya yake ilikua ikiendelea vizuri mpaka siku ya jumapili alipozidiwa na kukimbizwa hospitali ya Temeke ambapo usiku wa kuamkia leo ndipo mauti yalipomkuta.
Tulipomuuliza kuhusu kazi alizoziacha marehemu Said alisemakua ndio kuna nyimbo moja ambayo imewakutanisha TMK Wanaume Family na Tip Top ambapo marehemu alihusika katika kumba wimbo huo. Kuhusu utaratibu wa mazishi Said amesema kua wamekubaliana kua yatafanyika kesho. Unaweza msikiliza zaidi Said Fella hapa Chini….
 
Habari imeandikwa na Eddie Sucre kwa msaada wa Sweetbert wa Zenji Fm.
ali kiba na diamond
Ni siku chache zimepita tangu tamasha la Serengeti Fiesta lifanyike, ambapo tulishuhudia baadhi ya wasanii wa hapa Bongo wakipata nafasi ya kushare stage na wasanii wakubwa wa Afrika kama Davido na Waje huku kutoka Marekani alikua ni msanii T.I.
Ni ukweli usiofichika kua Fista ya mwaka huu imekua gumzo kubwa hasa baada ya kutokea mzozani kuhusu nani mkali zaidi kati ya Ali Kiba. Japo kulikua hamna ushindani lakini mashabiki wa wasanii hawa wawili wamekua katika marumbano makali kuhusu alimfunika mwenzake.
Millard ayo kupitia Ayo Tv alipata nafasi ya kufanya mahojiano na Ali Kiba kuhusu wasanii waliofanya poa stejini na alikiba alianza kwa kusema ” Nilichelewa kufika sikuweza kuwaona kina Ommy Dimpoz, Vanessa na kina Young Killer lakini niliobahatika kuwaona wote wamefanya kazi nzuri, nilimkuta Waje na Panto walifanya vizuri japo ni nyimbo zao chache tunazijua ” akazidi kufunguka zaidi kwa kuwataja wasanii ambao anaona yeye walifanya vizuri ” Mr Blue amenifurahisha sana, WEUSI wamefanya kazi nzuri…. kina Diamond wamefanya kazi nzuri pamoja na Linah ”
Habari imeandikwa na Eddie Sucre kwa msaada wa Millard Ayo.


bob junior
Mahaba niue !….Gossip mpya ni kuwa actress anayekuja juu kwa kasi kama moto wa kifuu  Sabby Angel ambaye pia ni mwanamuziki wa kizazi kipya tayari anadaiwa kuwa kwenye dimbwi zito la mahaba na Bob Junior ambaye pia ni star wa Bongofleva na mmiliki wa Sharobaro Records.
Kwa mujibu wa chanzo makini toka kwa wawili hao kikizungumza naSwahiliworldplanet  jioni hii kimesema kuwa Sabby na Bob Junior wanapendana na mahaba yao yalianzia studio ya Bob Junior hivi juzi kati Sabby alipoenda kwa ajili ya issue zake za muziki ndio kila mmoja akamzimikia mwenzake.
Ukiachilia mbali hayo Bob Junior amekuwa akirusha comments na kuchat kimahaba na Sabby Angel kwenye mitandao ya kijamii hususani Instagram mfano mzuri ni pale Bob Junior alipomwandikia Sabby ujumbe mzuri wa kumtakia mema katika siku yake ya kuzaliwa. Bob Juunio aliandika “HAPPY BIRTHDAY MALI MTUU HII AKISOGEA MTU NAMCHINJA TAKE A BIG KISS FROM UR ONE & ONLY SHOMBESHOMBE BABY MWAAAAAHXX BUSU PAAA JUU LIKUFATE ULIPO @sabbyangel HAPPY BIRTHDAY… ”
Ni mda sasa tangu Bob Junior aachane na mke wake na kwa kipindi hicho chote haikua ikijulikana rasmi nani anatoka kimapenzi na star huyo mpaka wakati huu ambapo wameamua kuweka uhusiano wao wazi. Hope siku si nyingi endapo mahaba yakizidi tunaweza kuwaona wakifunga ndoa. Unaweza ona mawasiliano yao wanayofanya Insta kwa kutazama picha hapa chini
Habara kwa msaada wa SwahiliWorldPlanet na Eddie Sucre

Hapo Sabby aliweka picha ya Bob Junior na Bob Junior kuanza kuchombeza
Bob Junior hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya wakati Sabby kwasasa anatamba sokoni na filamu ya Siri Ya Giningi huku filamu yake mpya ya Moto Wa Radi ikitarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu kuanzia sasa.
WANAFUNZI wawili wa shule za msingi za Nyabisara (Murito) na Kerende Kata ya Kemambo wilayani Tarime, Mara wameumwa hadi kuondolewa nyama zao za miguu na mamba walipokwenda kuoga maji ya mto kwa nyakati tofauti.

Wanafunzi hao ni Penina Joseph Mangure  (11) wa darasa la nne Shule ya Msingi Nyabisara katika Kijiji cha Murito ambaye ni mtoto wa mwenyekiti wa kijiji hicho, Joseph Mangure na Stephano Stephano (11) pia wa darasa la nne Shule ya Msingi  Kerende.

Taarifa za wanafunzi hao kukutwa na mkasa huo zilifikishwa katika Kituo cha Polisi Nyangoto (Nyamongo) na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya, Lazaro Mambosasa.
Akizungumza hivi karibuni, baba  wa Penina alisema mwanaye  aliokolewa na wananchi baada ya kupiga kelele wakati akiwa ameshikilia nyasi zilizomsaidia kushindwa kutumbukizwa majini na mamba huyo ambaye alikwenda na kipande cha nyama ya mguu wa kushoto.

Kwa upande wake mtoto Stephano alidaiwa kukutwa na tukio hilo alipokuwa akioga maji ya mto huo wakati akichunga ng’ombe wa nyumbani kwao.

Mtoto huyo alifanikiwa kuokolewa na wasamaria wema alipokamatwa na mamba huyo baada ya kupiga kelele na kufanikiwa kumtoa mguu katika mdomo wa mamba lakini akiwa ameshamnyofoa kipande cha nyama mguu  wa kushoto pia.

Mwenyekiti huyo alisema tangu Januari hadi Oktoba mwaka huu, watu watano wa kijiji chake wameshapoteza maisha baada ya kuliwa na mamba kwa nyakati tofauti huku wengine takribani 100 wakijeruhiwa.
Pia mwenyekiti huyo alisema mto huo kupita katika makazi ya watu ni tatizo na kwamba kila mara wananchi wanapopatwa na adha hizo huwasilisha taarifa katika Halmashauri ya Wilayani Tarime kupitia kitengo cha wanyama pori kwa ajili ya kusubiri hatua zaidi.

Alimuomba Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu kuhakikisha inawafidia wote waliojeruhiwa au kupotezewa maisha na mamba hao.
  Watoto hao bado wanasota majumbani mwao baada ya tiba ya awali huku wazazi wao wakitafuta fedha ili wapelekwe Hospitali ya Bugando, Mwanza
Polisi mkoani Arusha yamuua kwa risasi mtuhumiwa Namba Moja wa milipuko ya mabomu katika mikusanyiko jijini humo na umwagiaji watu tindikali baada ya kujaribu kutoroka akiwa njiani kwenda kuonesha bomu alilokuwa amelificha maeneo ya Kondoa mkoani Dodoma.


Kiongozi wa  matukio ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa jina la Yahaya Hassani Omary ameuawa na jeshi la polisi wakati  akijaribu kukimbia.

Inaelezwa kuwa
Yahaya Hassan ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.


 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Arusha,SACP Liberatus Sabas (pichani) Alisema kuwa tukio hilo limetokea  Oktoba 19 mwaka huu majira ya saa tano na nusu  katika barabara ya Babati mkoani Arusha wakati  akijaribu kuwakimbia polisi.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki mbili zilizopita  huko mkoani Morogoro  mara baada ya kutafutwa kwa muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani Kondoa mkoani Dodoma  kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu mengine.

"Mtuhumiwa huyo alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani alikuwa hakai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani Morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyiwa mahojiano alisema ameficha mabomu mengine huko Kondoa na jana alikuwa akipelekwa kuonyesha ndipo alipotumia triki zake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga judo na kutaka kuwakimbia askari ndipo akapigwa risasi mbili"alisema Sabas.

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu  ili kuweza kuteketeza matukio ya uhalifu.

 Na Woinde Shizza-Arusha

Unordered List

Sample Text

x


Total Pageviews

Find Us On Facebook
 
X

.

(X) Plz Like Page Hii.

Popular Posts

Recent Posts


Text Widget